Nipe Tano kwa Afya

Nipe Tano kwa Afya ni ushirikiano kati ya Foundation for a Healthy Kentucky na Idara ya Elimu ya Kentucky ambao unawafahamisha wanafunzi wa Kentucky kwenye madarasa ya K-12 na wazazi wao kuhusiana na tabia tano za kiafya ambazo wanaweza kuziunda na kuzifuatilia kwenye majira yajayo ya joto ili kujiweka sawa kwa mafanikio katika mwaka ujao wa masomo.

Kiingereza

Kihispania

Kampeni ya “Nipe Tano kwa Afya” ya majira ya joto 2023 inawahamasisha wana Kentucky katika:

  1. Kutoa Kipaumbele katika shughuli na mazoezi ya kimwili.
    Shughuli na mazoezi ya kimwili za mara kwa mara ni moja ya vipengele muhimu sana katika ujumla wa afya yako. Shughuli za kimwili zinaboresha usingizi wako, afya ya ubongo na mawazo ya utambuzi na inapunguza hatari za saratani na magonjwa ya moyo. Mhimize mtoto wako ajitahidi kufanya mazoezi na shughuli za kimwili kwa dakika 60 kila siku.

  2. Jizoeze kula kiafya.
    Kuchagua vyakula kiafya ni muhimu sana, hasa kwa watoto na vijana kwa kadri wanavyokua. Kula kiafya kunapelekea kuwa na nguvu imara, mifupa yenye nguvu, misuli na meno imara, kuboresha afya ya akili na inasaidia mtoto kuwa na uzito mzuri kiafya na hivyo kuzuia magonjwa sugu. Mapumziko ya kipindi cha majira ya joto ni kipindi kizuri cha kufanya majaribio ya mapishi na aina ya vyakula ambavyo mtoto wako atavifurahia wakati wa mwaka wa masomo.

  3. Fuatilia magonjwa sugu kama pumu, fetma na kisukari.
    Ni muhimu kwa wazazi na watoto kujua dalili na ishara za maonyo za magonjwa fulani kama vile pumu, fetma (uzito kupita kiasi), na kisukari. Kupumua kwa shida na kukohoa ni mojawapo ya dalili mbili za kawaida za pumu, lakini magonjwa mengine siyo rahisi kuyatambua. Iwe ni kama kuwa na utaratibu wa kupimwa kiwango cha sukari kwenye damu au kuwa na mazoezi ya mara kwa mara kimwili, jitahidi kuongea na watoto wako sasa ili wawe tayari shule zitakapofunguliwa.

  4. Jitahidi wakati wote uwe umekamilisha chanjo zako.
    Jitahidi uwe umekamilisha miadi yote ya uchunguzi wa “uzuri wa afya yako” na pia daktari wa meno katika majira haya ya joto. Kutana na daktari wako wa watoto kuhakikisha kuwa mtoto wako ametimiza chanjo zake zote na pia aonane na daktari wa meno wa familia ili kuhakikisha anajizoesha kufuata tabia ya afya ya usafi wa mdomo.

  5. Dhibiti Msongo na Hisia.
    Watu wenye nguvu ya kujifunza na kutumia ujuzi wa hisia za kijamii wanakuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na misongo na changamoto za kila siku. Kujifunza hisia za kijamii ni utaratibu wa kujenga tabia ya kujidhibiti na ujuzi wa mawasiliano baina ya watu ambao ni muhimu shuleni, kazini na kwenye mafanikio maishani. Baadhi ya shughuli chache zinazoweza kujenga ujuzi huu ni pamoja na kupanga rangi michoro, kuandika taarifa za matukio yako, kutafakari kwa kina, na kusikiliza muziki. Mapumziko ya wakati wa majira ya joto ni wakati ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufuatilia na kufurahia. Tumia muda huu kutafuta njia zinazomsaidia mtoto wako akiwa na hasira, akiwa amepata maudhi, au akiwa hana raha.

Majibu kwa Maswali Yanayoulizwa Sana

 

Videos

 
Kampeni hii na nyenzo zinazohusiana na hii inaungwa mkono na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani (HHS) kama sehemu ya usaidizi wa kifedha wa jumla ya $798,333 huku takriban 80% ikifadhiliwa na CDC/HHS. Yaliyomo ni yale ya waandishi na si lazima yawakilishe maoni rasmi ya, wala uidhinishaji na CDC/HHS, serikali ya Marekani, Idara ya Elimu ya Kentucky au Jumuiya ya Madola ya Kentucky.