Boresha Kinga Yako Kentucky

Chukua hatua za kuwa na afya njema.

Kiingereza

Kihispania

Wana Kentucky wengi zaidi wanasumbuliwa na magonjwa sugu baada ya janga la Corona.

Takwimu zinaonyesha kuwa viwango vya magonjwa ya kisukari, fetma na magonjwa ya moyo vimeongezeka, hasa kati ya Wamarekani wenye Asili ya Afrika. Lakini, zipo njia za kupambana na haya magonjwa sugu na Corona.

Hivi ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya kuboresha kinga yako ya mwili na kuwa na kudumisha afya njema.


Pakua nyenzo hapa.

Kula Vizuri.

Jitahidi kula vyakula bora na tumia matunda na mboga za majani kwa wingi, protini isiyo na mafuta sana, na maziwa yasiyo na mafuta.

Tembea/Fanya Mazoezi.

Mazoezi ya mara kwa mara ni kitu muhimu katika kujenga afya yako. Inaboresha mfumo wa kinga mwilini na kulala kwako, afya ya ubongo na utambuzi kwenye kufikiria.

Hakikisha Umepata Chanjo Zote Unazostahili.

Chanjo zinauwezesha mwili wako kupambana na virusi siku za mbeleni.

Soma zaidi kuhusu chanjo na viboreshaji vya COVID-19.

Tafuta Mahali pa Chanjo Karibu Nami.

Weka utaratibu wa vipimo wa kila mwaka na uchunguzi wa magonjwa.

Vipimo vya kinga ya afya vya mara kwa mara kupitia kwa daktari na daktari wa meno vinaweza kupelekea kugunduliwa kwa uwezekano wa matatizo ya afya yakiwa kwenye hatua za awali. Pata vipimo vyote vya uchunguzi vinavyoshauriwa kwa umri wako. Hii ni pamoja na mamografia, vipimo vya utumbo mkubwa na puru, uzito wa mifupa, na satatani ya mapafu. Ugunduzi wa mapema unakupa nafasi nzuri yay a kupata matibabu sahihi, kwa haraka, na kuepuka hali ngumu ya ugonjwa. Kwa afya nzuri ya mdomo, CDC inapendekeza kumuona daktari wako wa meno angalau mara moja kwa mwaka.  

Kuwa na Uzito Mzuri Kiafya.

Kutunza uzito wako kunachangia kuwa na afya nzuri kwa sasa na kadri unavyoendelea kukua kiumri.

Kunywa Maji ya Kutosha.

Kunywa maji ni muhimu katika afya yako kwa ujumla na katika kuondoa tatizo la ukosefu wa maji mwilini. Kutokuwa na maji mwilini kunaweza kupelekea katika changamoto za kutoweza kufikiria vizuri, mabadiliko ya hisia, joto kali mwilini, ukosefu wa choo na pia kuleta matatizo ya figo.

Pata Usingizi wa Kutosha.

Utafiti unaonyesha kwamba kutokupata usingizi wa kutosha kunaathiri mfumo wa kinga mwilini. Kukosa usingizi wa kutosha kunahusishwa na baadhi ya magonjwa sugu, ikiwemo kisukari, moyo, fetma, na msongo wa mawazo.

Osha Mikono Yako.

Usafi wako binafsi unaweza kudhibiti kuenea kwa magonjwa. Osha mikono baada ya kutoka bafuni, kabla ya kutayarisha na kula chakula, na baada ya kazi zinazochafua mikono au ukirudi nyumabni toka nje.

Acha Kuvuta Sigara na Kutumia Sigara za Umeme.

Uvutaji sigara unadhuru kinga ya mwili na utasababisha mwili kushindwa kupambana na magonjwa.

Tumia Pombe kwa Kiasi.

Baada ya muda Fulani, unywaji usio wa kiasi unasababisha udhaifu katika mfumo wa kinga mwilini. Inaweza kupelekea kupata magonjwa ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya moyo, saratani, magonjwa ya akili, na kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya baridi na virusi.

Punguza Msongo.

Kupunguza msongo na wasiwasi ni njia nyingine ya kuimarisha mfumo wako wa kinga.  Msongo wa muda mrefu husababisha mfumo wa kinga kupunguza nguvu zake na chembe chembe zake kushindwa kufanya kazi vizuri.