COVID-19
Taarifa za Chanjo na Chanjo-Nyongeza
Tafuta Sehemu Wanapotoa Chanjo
Ongea na Daktari wako kuhusu chanjo na chanjo-nyongeza
Chanjo za Covid zimeshatolewa mara millioni 600 hapa Marekani na mara Bilioni 12 Duniani kote.
Kwa maana hiyo, kuna takwimu na taarifa za chanjo hizi kuliko zingine zozote katika historia ya mwanadamu. [1]
Angalia Namba:
-
Milioni 610
Zaidi ya chanjo milioni 610 zimetolewa kwa usalama hapa Marekani.
-
Bilioni 12
Zaidi ya chanjo bilioni 12 zimetolewa kwa usalama duniani kote.
-
Mara 50
Wenye miaka 65 au zaidi ambao hawajachanjwa wa uwezekano wa mara 50 zaidi kulazwa hospitali kwa ajili ya COVID-19.
-
Mara 32
Wenye miaka kati ya 50 na 64 ambao hawajachanjwa wa uwezekano wa mara 32 zaidi kulazwa hospitali kwa ajili ya COVID-19.
-
Asilimia 90
Kwa kupata angalau dozi mbili za chanjo kunasaidia kupunguza uwezekano wa kuwekewa mashine ya kupumulia au kifo kutokana na COVID-19.
-
Asilimia 95
Utafiti umeonyesha kwamba kwa kupata angalau dozi mbili za chanjo kunasaidia kukabili madhara ya COVID-19 kwa aslimia 95.
Chanjo za COVID-19 Zimejaribiwa kwa Makini Sana na Kuidhinishwa:
Utaalamu uliotengeneza chanjo za COVID-19 umekuwa kwenye maendeleo ya chanjo kwa Zaidi ya miaka 20. [4]
Chanjo za COVID-19 zimekuwa na raslimali zisizo na kikomo na historia kubwa kutoka Marekani na Serikali nyingi duniani.
Chanjo zimetolewa mara milioni 600 Marekani na mara bilioni 12 duniani kote.
Chanjo za COVID-19 ni Salama na Zenye Ufanisi wa Hali ya Juu:
Utafiti umeonyesha kwamba chanjo mbili zilizopo za COVID-19 zina ufanisi wa ailimia 95 dhidi ya COVID-19. [5]
Takwimu toka kwa makumi elfu ya watu waliochanjwa inaonyesha kuwa chanjo ni salama na ina madahara madogo ya pembeni. [6]
Taasisi za FDA (Chakula na Madawa) na CDC (Udhibiti wa Magonjwa) zinaendelea kukusanya takwimu kutoka kwenye dozi zaidi ya milioni 610 zilizotolewa kufuatilia maswala ya usalama na madhara ya pembeni ya chanjo.
Kampeni hii pamoja na nyenzo zote husika zinaungwa mkono na Kituo cha Udhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC) cha Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu (HHS), kama sehemu ya tuzo ya msaada wa kifedha wa jumla ya $1,060,234 ambazo zimetolewa na Idaya ya Afya na Huduma za Kibinadamu. Yaliyomo ni kutoka kwa waandishi, na hayawakilishi maoni rasmi, au kuthibitishwa na CDC/HHS, Serikali ya Marekani, Baraza la Afya na Huduma za Familia Kentucky, au Jimbo la Kentucky.
Sources:
[1] https://ourworldindata.org/covid-vaccinations?country=OWID_WRL
[2] https://usafacts.org/visualizations/covid-vaccine-tracker-states/?utm_source=google&utm_medium=cpc&utm_campaign=ND-COVID-Vaccine&gclid=Cj0KCQjwguGYBhDRARIsAHgRm4-wlQotjOzju9b2JNYinwdAcfqrS84zAj5k03KZ0on2iUPQp1mkxosaAlzuEALw_wcB
[3] https://www.reuters.com/world/the-great-reboot/living-with-covid-where-pandemic-could-go-next-2022-08-01/
[5] Center for Disease Control
[6] Johns Hopkins University Medicine - https://www.hopkinsmedicine.org/health/conditions-and-diseases/coronavirus/is-the-covid19-vaccine-safe